Tanzania Ministry of Transport The United Republic of Tanzania, Ministry of Transport Miaka Hamsini ya Uhuru 1961-2011

News, Events, Speeches and Statements

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatoa tahadhari ya Mvua Kubwa na Upepo Mkali

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa Umma kuhusu Mvua kubwa inayotegemea kunyesha maeneo ya Ukanda wa Pwani, Visiwa vya Unguja na Pemba na Mikoa ya Kusini kuanzia tarehe 08 - 11 Oktoba, 2012. Mvua hizo zinategemea kuambatana na Upepo mkali.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo na kusainiwa na Mkurugenzi wake Dkt. Agnes Kijazi, Mvua hizo zinategemea kuambatana na upepo mkali. Taarifa hiyo ilitoa tahadhari kwa Mikoa ya Ukanda wa Pwani ( Dar es Salaam, Pwani na Morogoro), Visiwa vya Unguja na Pemba na Mikoa ya kusini (Mtwara na Lindi).

Kwa taarifa zaidi, tafadhali fungua hapa chini:Source: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)